Habari Mseto

Polisi ammininia risasi mwenzake na kumuua

November 11th, 2020 1 min read

GEORGE MUNENE NA FAUSTINE NGILA

Afisa wa polisi alimuua mwezake kwa kumpiga risasi kwenye mazingira yasiyoelekweka kwenye kiwanda cha kahawa cha Gathambi Kaunti ya Kirinyanga.

Wakazi walisema kwamba wwili hao walianza kuzozana kwasasabu  sizizojulikana walipokuwa wakilinda kiwanda hicho.

Wakati wawili hao walikuwa wanazozana ndio mmoja alipigwa risasi.

Mfanyakazi wa kiwanda Patrick Karani hicho alisema kwamba alisikia mlio wa risasi na alipokimbia eneo la tukio alipata mwathiriwa akiwa amelala ndani ya ndamu mingi.

Mfanyakazi mwingine Gerald Muriithi ,alisema kwamba alishuku mmoja wa maafisa hao wawili alikuwa amelewa wakati mzozo huo ulitokea.

“Mmoja wa afisa uwa anahubiri eneo hili hivyo tuliposikia kwamba alihusika kwenye vita ya bunduki tulishangaa,’alisema mmoja wa mkazi.

Mkuu wa polisi wa Kaunti ya Kirinyaga Magharibi Joseph Mwika alisema wamba afisa aliyehusika kwenye mahuaji alikamatwa na kupelekwa kwenye kituo cha polisi cha Baicho na mwili waaliyefariki ukapelekwa  kwenye chumba cha kuhifadhi maiti cha Kibugi.

“Hatujui kilichotokea kati ya maafisa hao wawili kabla ya mmoja kupiga risasi mwingine,”alisema huku akiomba wakazi wasaindie polisi kwenye uchunguzi.