Habari Mseto

Polisi ampiga mkewe risasi mara sita baada ya farakano

August 23rd, 2020 1 min read

NA CHARLES WANYORO

Mwanamke wa miaka 22 yuko katika hali mahututi kwenye Hospitali Kuu ya Kenyatta yake baada ya kupigwa risasi mara sita na mpenziwe ambaye ni afisa wa polisi wa Igembe Kaskazini, Kaunti ya Meru.

Afisa huyo, David Nyamweya, anasemekana kumwita mwanamke huyo kwenye kituo cha polisi cha Laare ambapo alimmininia risasi nje ya kituo hicho baada ya mzozo kuchacha.

Alikuwa tayari amempiga risasi ya tumboni na mguuni wakati wenzake waliingililia na kumpokonya bunduki.

Polisi aliyeshuhudia kisa hicho kilichotendeka Jumamosi usiku alisema kwamba mwezake aliomba ruhusa kufika chumbani kwake akisema kwamba alikuwa anaenda kuchukua koti.

Alienda Laare ambapo alikutana na mpeziwe walipozozana na mwishowe farakano hilo likazua mauti. “Alikuwa na sare zote za polisi na bunduki aliposafiri kwenda Laare,” alisema afisa huyo.

Maafisa wa polisi walimpeleka mwanamke huyo kwenye hospitali ya Meru kisha akatumwa Hospitali Kuu ya Kenyatta.

Naibu kamanda wa polisi wa kaunti hio Charles Langat alithibitisha kisa hicho lakini mkuu wa polisi Apolo Busolo alidinda kutaja kama afisa huyo alikamatwa au la.

TAFSIRI: FAUSTINE NGILA