Habari Mseto

Polisi anayechunguza kesi ya Alai aitwa kortini

July 17th, 2019 1 min read

Na RICHARD MUNGUTI

AFISA anayechunguza kesi inayomkabili mwanablogu matata Robert Alai aliamriwa afike kortini Julai 30 kutoa maelezo kuhusu kesi inayomkabili ya kuchapisha picha za maafisa wa polisi waliodunguliwa na kilipusi kaunti ya Wajir.

Hakimu mwandamizi Bw Kennedy Cheruiyot alitoa agizo hilo baada ya kuelezwa na kiongozi wa mashtaka kwamba “faili ya polisi haijawasilishwa kortini.”

Mahakama ilikuwa imetenga kesi ya Alai itajwe Jumanne ndipo mahakama ielezwe ikiwa amekabidhiwa nakala za ushahidi.

Hakimu alikubalia ombi la kiongozi wa mashtaka na kumtaka afisa anayechunguza kesi hiyo afike kortini kueleza sababu hakumkabidhi mshtakiwa nakala za mashahidi aandae ushahidi.