NA JOSEPH WANGUI
ALIYEKUWA afisa wa polisi Fredrick Leliman amehukumiwa kifo kwa kuua wakili Willie Kimani na watu wengine wawili.
Polisi wenzake Stephen Cheburet na Sylvia Wanjiku wamehukumiwa kifungo cha jela miaka 30 na 24 mtawalia.
Naye mpelelezi wao nje ya kitengo cha polisi Peter Ngugi amesukumwa jela miaka 20.
Wanne hao walipatikana na hatia mnamo Julai 22, 2022.
Jaji Jessie Lessit, ambaye sasa ni Jaji wa Mahakama ya Rufaa, aliwapata na hatia ya kumuua wakili Willie Kimani, mteja wake Josephat Mwenda na dereva wa teksi Joseph Muiruri mnamo Juni 23, 2016. Miili yao ilitupwa mtoni katika eneo la Ol Donyo Sabuk.
Jaji Lessit amesema Leliman ndiye alikuwa mpangaji mkuu wa unyama huo.
Wajane wazungumza baada ya hukumu kutolewa.