Habari Mseto

Polisi taabani kwa kumuua mshukiwa

October 13th, 2020 1 min read

NA BENSON AMADALA

 

Polisi wamelaumiwa kwa kumkamata, kumdhulumu na kumuua mshukiwa kwenye kituo cha polisi cha Mbururu kaunti ndogo ya Likuayani kaunti ya Kakamega. Mwili wa mshukiwa huyo ulipatikana Mto Nzoia.

“Mshukiwa huyo Dennis Lusava alikamatwa Oktoba 7 ,2020 na maafisa wa polisi kutoka kwa kituo hicho,” lilisema shirika la ILMU.

Mkurugenzi wa IMLU  Peter Kiama alisema: “Tunataka kujua kilichotokea kukamatwa, kufungwwa, kudhulumiwa, kupotea na kifo cha Dennis Lusava.”

IMLU pia imeweka stakabathi za kesi 24 ambazo washukiwa wanakisiwa kudhulumiwa na kuuwawa na polisi kuanzia Januari mwaka huu wa 2020.

Mwili wa mshukiwa huyo ulipelekwa kituo cha kuhifadhi maiti cha Webuye. Polisi walisema mshukiwa huyo alikuwa ameachiliwwa kwa dhamana.

Lakini wazazi wake walikana madai hayo wakisema kwamba wwalipomtembelea walipata akiwa bado amefungiwa akiwa amepigwa na kudhulumiwa akiwa hawezi kutembea.

Waliporudi kumwangalia tena hawakumpata kwenye kituo cha polisi. Walijulishwa na polisi kwamba walikuwa wamemwachilia.

Familia hiyo iliripoti mwanawe alikuwa amepotea na tukio hilo lilizua fujo hadi kituo hicho cha polisi kikachomwa.

TAFSIRI NA FAUSTINE NGILA