Polisi waanza kufanya uchunguzi baada ya moto kuchoma magari kwenye gereji

Polisi waanza kufanya uchunguzi baada ya moto kuchoma magari kwenye gereji

Na SAMMY KIMATU

MAGARI 13 yakiwemo ya kifahari yaliteketea katika gereji moja eneo la Cereal Board mkabala wa barabara ya Lunga Lunga, kaunti ndogo ya Makadara usiku wa kuamkia Jumatano.

Aidha, polisi walisema mamia ya wakazi kutoka mitaa ya mabanda karibu na eneo la mkasa walijaribu kupora mali ila polisi waliokuwa wamejihami waliwatimua na juhudi zao kugonga mwamba.

Mkuu wa polisi eneo la Makadara, Bw Timon Odingo alisema hasara ya thamani ya pesa isiyojulikana ilipatikana kufuatia kisa hicho cha moto.

Alieleza kwamba gereji iliyoteketea inamilikiwa na Bw John Kariuki na inajulikana kwa jina Donholm Earth Movers Garage.

Baadhi ya magari yaliyoteketea ni yakiwemo aina ya Mercedes Benz, Toyota, Datsun, X-Trail, Noah, Helium, Sprinter, Ranger, Wingroad, Nissan na Blue Bird.

Chanzo cha moto huo hakijulikani lakini polisi wameanzisha uchunguzi wao.

You can share this post!

Mchoraji vibonzo wa ‘Taifa Leo’ ang’aa

Samuel Eto’o kuwania urais wa Shirikisho la Soka la...