Polisi waanza uchunguzi baada ya ofisi ya ‘Jicho Pevu’ kuvamiwa

Polisi waanza uchunguzi baada ya ofisi ya ‘Jicho Pevu’ kuvamiwa

NA ANTHONY KITIMO

POLISI katika Kaunti ya Mombasa, wameanzisha uchunguzi kuhusu kisa ambapo afisi ya Mbunge wa Nyali, Bw Mohamed Ali, ilivamiwa usiku wa kuamkia jana.

Mkuu wa polisi wa Nyali, Bw Daniel Mumasaba, alithibitisha kisa hicho lakini akasema uchunguzi bado uko katika hatua za awali.

“Tumetafuta alama za vidole milangoni na tunakagua video za CCTV. Tuna matumaini tutawakamata washukiwa hivi karibuni,” akasema Bw Mumasaba.

Viongozi wa Kenya Kwanza eneo la Pwani, walilalamika kuwa hawapewi usalama wa kutosha wakati nchi inapojiandaa kwa uchaguzi wa Agosti 9.

Wakiongozwa na mwaniaji wa ugavana Mombasa kupitia chama cha UDA, Bw Hassan Omar, na wagombeaji wa viti wengine, walilalamika kuwa uvamizi wa afisi ya Bw Ali ni ishara tosha kuwa malalamishi yao ya muda mrefu kuhusu ulinzi wao hayatiliwi maanani.

“Tuna maswali mengi kwa kuwa afisi hiyo iko mita chache kutoka kwa afisi ya kamishna wa Kaunti Ndogo ya Nyali na inalindwa na polisi wa utawala,” akasema Bw Omar.

  • Tags

You can share this post!

Digrii: Afueni kwa Jumwa korti ikikataa ombi la kumzuia...

Mdahalo: Wawaniaji ugavana wafafanulia wakazi wa Kiambu...

T L