Habari Mseto

Polisi wachunguza kisa cha mauaji ya Kevin Omwenga

August 23rd, 2020 1 min read

NA VINCENT ACHUKA

Polisi wanachunguza kisa cha mwanaume mmoja aliyeuawa kwa kupigwa risasi Ijumaa Kilimani kisa kinachohusu  kashfa ya dhahabu .

Kevin Omwenga wa miaka 28 alipigwa risasi nyumbani kwake ghorofa  ya saba Galana Suite barabara ya Galana na mwanaume anayesemekana kuwa mlinzi wake baada ya mzozo unaosemekana kuhusu dhahabu ghushi.

Alitajwa kufariki baada ya kufikishwa hospitali ya Nairobi Women baada ya kupigwa risasi.

Maafisa wa upelelezi wanawatafuta waliokuwa na Bw  Omwenga mara ya mwisho,mausianaona ushirika miezi iliyopita ambayo duru za kuaminika zinasema kwamba alibadilisha Maisha aliyokuwa akiishi.

Bw Omwenga alikuwa ameajiriwa kazi ya kuuza magari kwenye kampuni ya Motor Bazaar Lavington kati  ya mwaka 2016 na mwaka jana ambapo Maisha  yake yalibandilika haraka akaanza kuishi maishaa ya kifahari.

Aliacha kazi na kuamia Galana Suites ambapo alikodisha  nyumba aliokuwa analipa Sh 150,000 kwa mwezi ,nyumba ambayo ina  samani kwa na pia akabadilisha marafiki. Mapema mwaka huu Bw Omwega alinunua gari aina ya Porsche Panamera  ambayo inagarimu Sh14 milioni.

TAFSIRI: FAUSTINE NGILA