Habari Mseto

Polisi wachunguza waliomuua mwanamke Tana River

August 13th, 2020 1 min read

 STEPHEN ODUOR na FAUSTINE NGILA

Polisi katika Kaunti ya Tana River wanachunguza kifo cha mwanamke mmoja ambaye mwili wake ulikatwa kichwa na kupatikana Jumatatu jioni eneo la Vibao Viwili kwenye barabara ya Malindi-Garsen.

Kamanda wa polisi Fredrick Ochieng alisema kwamba wakazi walijulisha polisi baada ya kupata mwili huo mita 500 kutoka kituo cha polisi cha Hurara na kichwa chake mita 20 mbali.

Walitambua mwathiriwa huyo wa miaka 58 kama Dumal Elema.

“Tulikuta damu kidogo kwa mwili na kidogo kando ya barabara .Hakukuwa na dalili ya ajali yoyote ama kusumbuka,”akiongeza kwamba mwanamke huyo anaeza kuwa aliuwa kwingine na kutupwa.

Mpwa wa mwathiriwa aliambia Taifa Leo kwamba alionekana kwenye bodaboda akielekea kwenye kiji cha Hurara baada ya kununua bidhaa kutoka kituo cha Hurara,nab bado mali huio yake ilikuwa bado kupatikana.

Mwendeshaji wa boda alihojiwa na badaye kuachiliwa. Polisi waliomba yeyote akona ujumbe awajulishe.

Mwili huo ulipelekwa kwenye cha kuhifadhi maiti cha Malindi.