Habari Mseto

Polisi wakamatwa wakinywa chang'aa

October 20th, 2020 1 min read

NA FAUSTINE NGILA

Maafisa watatu kutoka kituo cha polisi cha Ugunja Kaunti ya Siaya wamekamatwa walipokuwa wakikunywa pombe  haramu  ya Chang’aa kazini.

Maafisa hao walipatikana wakiwa na pombe hiyo vyumbani vyao ndani ya kituo hicho cha polisi Jumapili.

Kamanda wa polisi wa Kaunti ndogo ya Ugunja  Bw Lazarus  Tarus aliripotiwa kuingia nyumbani kwa maafisa hao ambapo maafisa hao waikuwa wamejificha.

Afisa aliyeshuudia hayo alisema wezake walionywa dhidi ya tabia zao na afisa mwenzake waache tabia hizo  lakini wakakaidi.

“Walikamatwa mara hiyo hio na kufungiwa kwenye kituo cha polisi cha Ugunja ,”afisaa huyo aliambia Taifa Leo.

Afisa mmoja alikuwa amehamishwa kazi kutoka kituo cha polisi cha Ruwe hadi kituo cha Simunya lakini akakosa kuripoti kwenye kituo hicho.