Habari Mseto

Polisi wamnasa mama wa kanisa aliyenyofoa nyeti za mumewe

August 27th, 2018 1 min read

Na Sammy Kimatu

MWANAMKE anayedaiwa kunyofoa sehemu nyeti za mumewe akiwa usingizini katika mtaa wa mabanda wa Mukuru-Kaiyaba, South B, Kaunti ya Nairobi hatimaye amekamatwa.

Polisi wamemfungia katika kituo cha polisi cha Industrial Area kwa mahojiano kuhusiana na kisa hiki.

Mshukiwa, Bi Esther Namale ambaye ni mama wa kanisa, anadaiwa kumtendea mumewe unyama huo usiku wa kuamkia Ijumaa.

Japo wamekaa kwa ndoa kwa miako 20, majirani wao walisema wawili hao wamekuwa wakizozana mara kwa mara wakiwa mtaani.

Mshukiwa alikwepa mtego wa polisi kukamatwa alipopashwa habari kwamba polisi walikuwa njiani wakija kumtia mbaroni. Alihepa siku ya Ijumaa huku polisi wakiapa kumtafuta kwa udi na uvumba.

Duru za polisi zilieleza kwamba mwanamke huyo alifichwa katika mtaa wa Makongeni.

Baada ya runinga ya NTV kuangazia kisa hicho katika habari za saa saba mchana, mara mora polisi walitumwa kumsaka na kumnasa mshukiwa.