Habari Mseto

Polisi wamsaka mwalimu aliyotoroka karantini

November 12th, 2020 1 min read

NA FAUSTINE NGILA

Polisi mjini Mumias wanamtafuta mwalimu aliyetoroka kutoka kwa kituo cha kujitenga cha corona.

Dkt Paul Wangwe  ambaye anahusika na kituo cha kutenga wagonjwa wa corona kwenye hospitali ya Mumias aliripoti kwamba mgonjwa kwa jina Violet Shamala wa miaka 36 mkazi wa Kijiji cha Ingotse Kaunti ya Kakamega alihepa Novemba 4.

“Alitoroka bila idhini ya maafisa wa afya. Alikuwa anaendelea kupata nafuu lakini bado anaweza kusababisha maambukizi,’ alisema Dkt Wagwe.

Mkuu wa Polisi wa eneo hilo Paul Kipkorir alisema kwamba bado wanamtafuta mwalimu huyo.