Habari Mseto

Polisi wamsaka mwenzao kuhusu mauaji

August 13th, 2020 1 min read

RUTH MBULA na FAUSTINE NGILA

Polisi Kaunti ya Kisii wanatafuta mwenzao Eunice Achieng Okal ambaye alionekana mara ya mwisho Juli 30.

Konstebo Achieng, ambaye alikuwa anafanya kazi kwenye kituo cha polisi cha Nyanchwa aliomba siku moja ya mapumziko Julai 29, akisema kwamba alikuwa atembelee nyanya yake mgonjwa anayeishi Kaunti ya Migori

Uchunguzi ulisema kwamba hakutembelea nyanyake lakini alikutana na mumewe wa zamani John Odiango mjini Kisii.

Lakini Bw Odiango alipatikana amefariki nyumbani kwake Oyugis kaunti ya Homabay Agodsti 7 kile ambacho kinaaminika kuwa kujitoa uhai.

Kamanda wa polisi wa kaunti ya Kisii Jebel Munene alisema kwamba afisa huyo wa polisi alikuwa arudi kazini Juli 31.

Ripoti zilisema kwamba Bi Acchieng na bwana huyo wa zamani walikutana Kisii kukamilisha dili mabayo alikuwa apate 250,000 kutoka kwake kutoka kwa biashara waliomiliki pamoja.

Wakati Bw Odiango alikuwa akifanya ripoti ya kupote kwa mwanaao alipokea simu kwamba alikonekana Oyugis na alikuwa na mwonekano wa mwendawazimu.

“Walimtafuta hadi usiku lakini hawakumuona.Mwili wake ulipatakina ukininginia kwenye paa siku iliyofuta.Nguo zake zilipatikana zimetupwa kwa jirani,”Habari kutoka kwa polisi zikisema kwamba leso ya bibi wake wa kitambo lilitumika kumnyonga.