Polisi wanne wanaoshtakiwa kwa mauaji wapatwa na Corona wakiwa jela

Polisi wanne wanaoshtakiwa kwa mauaji wapatwa na Corona wakiwa jela

Na RICHARD MUNGUTI

MAHAKAMAU kuu ilifahamishwa Alhamisi maafisa wanne wa polisi kati ya sita wanaoshtakiwa kuwaua ndugu wawili kaunti ya Embu wameambukizwa ugonjwa wa Covid-19.

Sasa wako karantine katika gereza kuu la kamiti.Hivyo basi Koplo Benson Mbuthia Mabuuri na Makonstebo Martin Musamali Wanyama, Nicholas Sang Cheruiyot na James Mwaniki Njohu hawakufika kortini.

Walifuata kesi hiyo kwa njia ya mtandao.Waliofika mbele ya Jaji Daniel Ogembo ni Koplo Consolata Njeri na KonsteboLilian Cherono Chemuna.Maafisa hao sita wanakabiliwa na shtaka la kuwaua Emmanuel Mutura and Benson Njiru mnamo Agosti 1,2021 katika eneo la Kianjakoma , kaunti ya Embu.

Lakini ombi lao la kuachiliwa kwa dhamana halikusikizwa kwa vile chama cha mawakili nchini (LSK), shirika la kutetea haki za binadamu la IMLU, mamlaka huru ya utenda kazi ya polisi (IPOA), shirika la kitaifa la kutetea haki za binadamu (KNHRC), Shirika la kimataifa la kutetea haki (IJM) viliomba vikabidhiwe nakala za ombi hilo la dhamana.

Lakini Bw Omari alishutumu hatua hiyo akisema “kile mashirika hayo ya kutetea haki za binadamu yanavyotaka ni kuhusishwa katika kesi hiyo kwa lengo la kusaka pesa kutoka mashirika ya ng’ambo.”

Jaji Ogembo aliahirisha kesi hiyo hadi leo atakaposikiza ombi hilo la dhamana.IMLU iliomba ombi lisikizwe baada ya wiki moja lakini mahakama ikakataa.

  • Tags

You can share this post!

Itumbi yuko na kesi ya kujibu katika dai kulikuwa na njama...

GWIJI WA WIKI: Fred Mutwiri