Polisi wapokea mafunzo jinsi ya kukabili ufisadi

Polisi wapokea mafunzo jinsi ya kukabili ufisadi

Na TITUS OMINDE

TUME ya Maadili na Kupambana na Ufisadi (EACC) Kaskazini mwa Rift Valley, imetoa mafunzo kwa zaidi ya maafisa 20 wakuu wa polisi kutoka Uasin Gishu, kuhusu masuala ya maadili na ufisadi miongoni mwa maafisa.

Kamanda wa Polisi Kaunti ya Uasin Gishu, Ayub Gitonga, alisema mafunzo yalilenga kubadili dhana potofu kwamba polisi ndio fisadi zaidi nchini.Akizungumza wakati wa mafunzo hayo katika kituo cha polisi cha Eldoret Central jana, Kamanda wa Polisi Kaunti ya Uasin Gishu Ayub Gitonga alisema, mafunzo hayo yalilenga kupinga dhana potofu kwamba taasisi ya polisi ndio fisadi zaidi serikalini.

“Kuna dhana potofu kwa umma kwamba maafisa wote wa polisi ni wafisadi, hii ndiyo maana nimewaalika maafisa wakuu wote wa polisi katika kaunti hii kwa mafunzo haya ya EACC ili kuwawezesha maafisa wetu kuelewa jukumu lao katika vita dhidi ya ufisadi,” akasema Bw Gitonga.

Bw Gitonga alisema kuwa haikuwa haki kuainisha polisi kuwa mojawapo ya taasisi fisadi zaidi za kiserikali wakati wengi wa maafisa hao hawana taarifa sahihi za jinsi ya kupigana na rushwa katika utekelezaji wa majukumu yao“Pamoja na kuwa na sheria za rushwa kuna haja ya afisi ya EAC kuelimisha maafisa wetu ili kuunga mkono vita dhidi ya ufisadi,” akasema Bw Gitonga.

Alisema kampeni hiyo ni miongoni mbinu za mafunzo kuimiarisha ushrikiano kati ya polisi na tume hiyo.

You can share this post!

Vijana wengi kuwania 2022 viti vyeo 2022

Daktari asema hakupata sumu katika mwili wa Tecra

T L