Polisi wasaka walioua mtu kwenye baa

Polisi wasaka walioua mtu kwenye baa

NA KENYA NEWS AGENCY

POLISI kaunti ya Homa Bay wanachunguza kifo cha mwanaume wa umri wa makamo aliyedungwa kisu Jumamosi katika baa moja huko Kaksingiri, eneo bunge la Suba Kusini.

Chifu wa Kaksingiri, Bw Daniel Magadi, aliwaomba wanakijiji wajitokeze ili kuwasaidia polisi na uchuguzi.

Kwingineko, chifu wa Kasewe eneo bunge la Rachuonyo Mashariki, Bw Moses Ongere alimwaga lita 4,000 za pombe ya aina ya kangara ma 40 za pombe haramu katika operesheni ya kuzuia utengezaji na uuzaji wa pombe aina hiyo kwenye eneo hilo.

  • Tags

You can share this post!

ALI SHISIA: Kiswahili kama chombo cha umoja na maendeleo...

Majonzi afisa akiua mpenziwe kisha kujiangamiza kwa risasi

T L