Habari Mseto

Polisi wawili motoni kwa kumuua mshukiwa

October 2nd, 2020 1 min read

NA JOSEPH OPEDA

Polisi wawili wamekamatwa kwa kumpiga mshukiwa hadi kifo Kaunti ya Nyandarua. Polisi hao wanaohudumu kwenyye kituo cha  polisi cha Malewa waliotambulika kama Wilson Irungu na George Otrieno walikamatwa kwa mauaji ya David Wachira aliyefariki mwaka mmoja uliopita alipokuwa  kizuizini, lilisema shirika la IPOA.

Mwenyekiti wa shirika hilo Anne Makori  alisema kwamba wawili hao walikamatwa baada ya afisi ya mashtaka kuthibitisha kukamatwa kwao.

Mwathiriwa alikuwa amekamattwa kwa makosa ya kuiba ng’ombe Aprili 20 na akafariki siku iliyofuatiaa kwenye hospittali ya Olkalou.

Polisi mkuu alikuwa amesema kwamba alifariki baada ya kunyongwa na chakula alipokuwa akila kwenye kituo cha polisi.

Lakini shirika hilo la IPOA lilifanya uchunguzi na kubaini kwamba alifariki kutokana na kichapo alichopewa na maafisa hao wa usalama.

Bi Makori alisema kwamba waliochunguza kisa hicho walibaini kwamba mshukiwa huyo alifariki kutokana na maumivu makali alipokuwa amezuiliwa kwenye kituo cha polisi.

“Ipoa waliomba afisi ya mashtaka ya umma iwashtaki wawili hao kwa makosa ya mauaji. Afisi hiyo ilikubaliana na wito huo wa shirika hilo Agosti 1 ,” ulisema ujumbe huo.

Bi Makori alithibitisha kwamba maafisa hao walipelekwa Naivasha kwa uchunguzi wa kiakili.

TAFSIRI NA FAUSTINE NGILA