Dondoo

Polo aliyeacha dirisha wazi kurina asali ya kando afumaniwa na mpenzi

February 24th, 2019 1 min read

Na TOBBIE WEKESA

DANDORA, NAIROBI.

Kioja kilizuka kwenye ploti moja mtaani hapa baada ya kipusa kumfumania mchumba wake akila uroda na mpango wa kando.

Inasemekana demu alimpata polo juu ya mzinga akichovya asali huku dirisha likiwa wazi.?

Duru zinasema kipusa alikuwa na wasiwasi kwa sababu hakuwa amewasiliana na polo siku nzima.

Kulingana na mdokezi, simu ya polo ilikuwa mteja na akaamua kwenda hadi alikoishi kubaini kilichokuwa kikiendelea. ? I

nadaiwa alipofika kwa mlango wa nyumba ya jamaa, alikaribishwa na viatu vya kidosho aliyekuwa chumbani.

Inasemekana mwanadada aliamua kujitupa ndani ya nyumba mara moja. Jamaa alisikia sauti ya mlango ukisukumwa lakini akafikiri ni paka aliyependa kuwasumbua.

Kipusa alifululiza moja kwa moja hadi chumba cha kulala cha polo na kumpata juu ya mzinga.? “Huyu ni nani,” alimfokea jamaa alipompata na kidosho kitandani naye jombi akashindwa la kusema. “Nauliza huyu ni nani na mnafanya nini,” mwanadada alimkaripia jamaa.

Inadaiwa jombi alianza kugugumiza maneno. ? Duru zinasema kipusa alichukua kufuli kisha akachomoka nje na kuwafungia ndani ya nyumba huku akiwashambulia kwa maneno.

“Huwezi kunitumia kama karatasi shashi hivi. Leo ujanja wako umefika mwisho. Mwizi leo hana lake,” kipusa alifoka. ? Inadaiwa polo alijaribu kumrai demu aufungue mlango lakini wapi.

“Uliamua kuifunga simu kumbe haya ndiyo mambo unafanya, basi endeleeni,” alimkaripia jamaa. ? Wenyeji kwenye ploti walibaki kutazama sinema iliyokuwa ikiendelea.

“Hata kama ni njaa ya tunda. Jana nilikuwa hapa, nikampa uroda mpaka akasema ametosheka. Sasa anafanya nini, fisi huyu” kipusa aliteta.

Duru zinasema mrembo alikataa kabisa kuufungua mlango hadi landilodi akaitwa kumshawishi.