Dondoo

Polo asaka chips funga aliyehepa na pesa zake

March 24th, 2024 1 min read

NA JANET KAVUNGAP

Bombolulu, Mombasa

POLO mmoja mtaani hapa anamsaka mwanadada aliyetoroka baada ya kuiba pesa zake muda mfupi baada ya kurushana roho.

Inasemekana msupa alikuwa ameenda nyumbani kwa jamaa alipozitupia jicho noti zilizowekwa juu ya meza.

Kulingana na mdokezi, jamaa alikuwa amemrushia chambo na akameza.

Baada ya shughuli, jamaa aliingia bafu na demu akapata fursa ya kuchomoka na noti na kutoroka.

Jamaa alipotoka bafu hakumpata mama na pesa alizoweka juu ya meza.

Alitoka nje na kuwauliza watu iwapo walikuwa wamemuona mwanadada huyo ambaye tangu kisa hicho hakuonekana tena mtaani na jamaa akaapa kumsaka.