Dondoo

Polo mjanja apeleka mamanzi kibandani badala ya hotelini

April 27th, 2024 1 min read

NA NICHOLAS CHERUIYOT

NAROK MJINI

POLO wa hapa alifanya uamuzi wa haraka kuepuka hasara kwa kuwapeleka vipusa wanne walioandamana na demu wake kibandani badala ya hoteli aliyopanga kujivinjari na mpenzi wake.

Kulingana na duru, polo alimpigia simu demu wake akimtaka wakutane hoteli ya kifahari wafurahie mlo lakini akaduwaa alipofika na wasichana wengine wanne.

“Twende tuwainue mahasla kwa kula chakula chao. Ninapenda vile wanajituma kazini,” polo aliarifu vipusa hao.

Baadaye vipusa walisikika wakiteta kukosa minofu naye jombi akaarifu wenzake kuwa alikwepa mtego wa bili kubwa kiujanja.