Habari Mseto

Prof Kiama aanza kazi rasmi Chuo Kikuu cha Nairobi

June 5th, 2020 1 min read

NA FAITH NYAMAI

Profesa Stephen Kiama ameapishwa kuwa Naibu Chansela wa Chuo Kikuu cha Nairobi wa nane.

Hii inakuja miezi kadhaa baaya ya kuchaguliwa kwake na kupuuzwa na Waziri ya Elimu Profesa George Magoha.

Sherehe hiyo ilifanyika kupitia mitandao huku wafanyakzi wa chuo hicho na wanafunzi wakifuatiliaa kupitia mitandaoni. Profesa Kiama aliteuliwa Januari 6 na baraza la chuo hicho inayoongozwa na Profesa Julia Ojiambo.

Akiongea baada ya kukabidhiwa mamlaka alisema: “Nitajitahidi nifanye kulingana na uwezo wangu kukukifanya chuo hiki kuwa bora.”

“Profesa Kiama, wewe ni bora miongoni mwa mengine, sasa kazi ianze,” alisema Profesa Ojiambo huku akiwahimiza wafanyakazi wa chuo hicho kufanya kazi kwa pamoja.