Habari

Prof Kiama kuendelea kuwa Naibu Chansela UoN

February 27th, 2020 1 min read

Na ABIUD OCHIENG

PROF Stephen Kiama sasa ataendelea kuwa Naibu Chansela wa Chuo Kikuu cha Nairobi (UoN) baada ya Waziri wa Elimu George Magoha kuitupilia mbali barua iliyobatilisha uteuzi wake.

Waziri Magoha ameiambia mahakama ya masuala ya Leba, Nairobi mnamo Alhamisi kwamba ameiondoa barua hiyo iliyomvua cheo Prof Kiama.

Uamuzi huu wa kutupilia mbali barua umejiri baada ya waziri na Prof Kiama kusuluhisha tofauti baina yao nje ya mahakama jinsi pande zinazohasimiana zilivyokuwa zimeshauriwa.

Mwenyekiti wa Baraza la Uon Prof Julia Ojiambo, katika barua kwa wadau Januari 2020 alitangaza kuteuliwa kwa Prof Kiama kuongoza chuo kikuu hicho.

Magoha hata hivyo alitengua uteuzi huo na kumuelekeza Prof Mbeche awe kaimu Naibu Chansela.