Michezo

PSG mbioni kumsajili Sergio Ramos

May 9th, 2019 1 min read

MASHIRIKA NA JOHN ASHIHUNDU

PARIS, Ufaransa

Klabu tajiri ya PSG ya ligi kuu ya Ufaransa imo mbioni kumsajili Sergio Ramos kutoka klabu ya Real Madrid ambaye ndiye beki anayelipwa pesa nyingi zaidi duniani kwa sasa.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 33 amekuwa na Madrid tangu 2005 ambayo ameichezea zaidi ya mara 600, huku mkataba wake ukitarajiwa kumalizika msimu wa 2020-21.

Lakini ili mpango huo ufaulu, PSG nao wanapanga kumpiga bei beki wao, Thiago Silva, raia wa Brazil aliye na umri wa miaka 34. Ramos pia anawindwa na klabu ya Manchester United ya ligi kuu ya Uingereza (EPL).