Michezo

PSG wala kadi mbili nyekundu na kuzamishwa 2-0 na RB Leipzig kwenye UEFA

November 5th, 2020 1 min read

Na MASHIRIKA

RB Leipzig walitoka nyuma na kuwapepeta Paris Saint-Germain (PSG) 2-1 katika mechi ya Kundi H ya Klabu Bingwa Ulaya (UEFA) mnamo Novemba 4, 2020.

Ushindi kwa Leipzig kutoka Ujerumani uliwawezesha kufikia Manchester United kwa alama sita baada ya vijana hao wa kocha Ole Gunnar Solskjaer kupigwa 2-1 na Istanbul Basaksehir nchini Uturuki.

Angel Di Maria aliyepoteza penalti, aliwaweka PSG kifua mbele kunako dakika ya sita kabla ya Christopher Nkunku kusawazisha dhidi ya waajiri wake wa zamani.

Emil Forsberg aliwaweka Leipzig uongozini kupitia penalti ya dakika ya 57 kabla ya kiungo wa zamani wa PSG, Idrissa Gueye na beki Presnel Kimpembe kuonyeshwa kadi nyekundu kwa upande wa PSG. Miamba hao wa Ufaransa ambao kwa sasa wanatiwa makali na kocha Thomas Tuchel, wana alama tatu pekee.

Moise Kean anayechezea PSG kwa mkopo kutoka Everton, ndiye mwanasoka wa pekee aliyeridhisha zaidi kwa upande wa kikosi cha mkufunzi Tuchel.

Leipzig walishuka dimbani wakitawaliwa na kiu ya kujinyanyua baada ya kupokezwa kichapo cha 5-0 katika mechi yao iliyopita dhidi ya Man-United ugani Old Trafford.