PSG warejea kileleni mwa jedwali l

PSG warejea kileleni mwa jedwali l

Na MASHIRIKA

PARIS Saint-Germain (PSG) walirejea kileleni mwa jedwali la Ligi Kuu ya Ufaransa (Ligue 1) baada ya kupepeta Angers 1-0 Januari 16, 2021.

Bao la pekee na la ushindi kwa upande wa PSG lilipachikwa wavuni na Layvin Kurzawa katika kipindi cha pili. Ushindi huo uliendeleza rekodi ya kutoshindwa kwa PSG katika jumla ya mechi saba mfululizo.

Kocha Mauricio Pochettino wa PSG hakusimamia mchuano huo kwa kuwa anaugua Covid-19, tukio litakalomweka nje ya mechi mbili zijazo zitakazosakatwa na waajiri wake.

PSG ambao ni mabingwa watetezi wa taji la Ligue 1, sasa wanaselelea kileleni mwa jedwali kwa alama 42, mbili zaidi kuliko nambari mbili Olympique Lyon ambao wana mchuano mmoja zaidi wa kusakata ili kufikia idadi ya mechi 20 ambazo zimetandazwa na PSG hadi kufikia sasa.

Katika mchuano mwingine wa Ligue 1 uliosakatwa Jumamosi usiku, limbukeni Nimes walizamisha chombo cha Olympique Marseille kwa ushindi wa 2-1 ugenini.

TAFSIRI NA: CHRIS ADUNGO

You can share this post!

Hatimaye Ozil aondoka Arsenal

KPA na Equity Bank kuwakilisha Kenya kwenye vikapu Afrika