Raia mwingine wa kigeni apatikana amefariki ndani ya meli Mombasa

Raia mwingine wa kigeni apatikana amefariki ndani ya meli Mombasa

Na ANTHONY KITIMO

MAAFISA mnamo Jumanne waliondoa mwili wa mwanamume aliyefariki ndani ya meli iliyotia nanga katika bandari ya Mombasa, ili ukafanyiwe upasuaji kubaini chanzo cha kifo chake.

Shan Syed Tasawar, 55, raia wa Pakistan alisemekana kufariki siku tano zilizopita wakati meli ya Mv MSC Alice ikikaribia kufika bandarini.“Baharia huyo alipatikana amepoteza fahamu na juhudi za kumwokoa hazikufua dafu.

Alithibitishwa kufariki katika hospitali ya meli hiyo alikokimbizwa kwa matibabu,” sehemu ya ripoti ya polisi ilieleza.Shughuli za kupakua mizigo katika meli hiyo Jumanne zilicheleweshwa kwa muda maafisa kutoka kitengo cha baharini, afya mpakani, uhamiaji na ajenti wa kampuni inayosimamia meli hiyo walikuwa wakikagua eneo la mkasa.

Mwezi jana kisa kingine kama hicho kiliripotiwa baada ya Samson Samuel Bensley, 52, raia wa India kupatikana amefariki ndani ya meli ya kusafirisha mizigo ya Mv Pine Arrow. Ripoti ya polisi ilisema kuwa alikumbwa na mshtuko wa moyo.

You can share this post!

Jamii yalalamika kutatizwa na operesheni ya usalama Boni

Corona: Watu 700,000 kufariki Ulaya katika miezi minne ijayo

T L