Habari Mseto

Raia wa kigeni wanaswa kuhusu biashara ya kulangua watu

October 19th, 2020 1 min read

NA WAWERU WAIRIMU

POLISI Kaunti ya Isiolo wamewazuilia raia wawili wa kigeni waliokamatwa maeneo ya Merti na Garbatulaa siku tatu ziliopita kwa kuwa humu nchini kinyume na sheria.

Maafisa hao pia walikamata waendeshaji bodaboda 12 ambao walisemekana kuwa wanahusika kwenye biashara haramu za kuwalangua watu.

Polisi waliwakamata maeneo ya Biliqo Merti Jumamosi usiku. Waendeshaji bodaboda pia 13 walikamatwa huku mmoja akihepa.

“Washukiwa hao wanazuiliwa kwenye kituo cha polisi cha Merti na watafikishwa kortini Jumatano ,” alisema naibu kamishena wa kaunti Salim Bagana.

Biashara ya kulangua wananchi imekuwaa ikipungua huku wendesdhaji biashara hiyo haramu wakitumia barabara zenye zinapitia vichakani za Yamina-Dogogicha.

Washukiwa hao wamekuwa wakiwasifirisha wananchi hao nje kuenda Merti kwa kutumia bodaboda na kurudishwa tena Isiolo na Nairobi.

Kituo hicho cha polisii cha Yamicha hakina maafisa wa usalama wa kutosha na hakina magari, hivyo ikiwazuia maafisa hao kuwawinda wanaoendesha biashara hiyo ya kuuza binadamu

“Tutashukuru kama maafisa wa polisi wataletwa eneo hili na kituo hiki cha polisi kipewe magari ili kurahisisha mambo,” alisema Bw Bagana.

Kamishena wa Kaunti Hermna Sahmbi aliwaonya wakazi wanaojihusisha na mabo ya uhalifu kwamba chuma chao ki motoni.

TAFSIRI NA FAUSTINE NGILA