Raia wa Uganda anayeshukiwa kumuua mke-mwenza ndani

Raia wa Uganda anayeshukiwa kumuua mke-mwenza ndani

NA JOSEPH NDUNDA

WAPELELEZI kutoka Idara ya Uchunguzi wa Uhalifu (DCI) wanamzuilia mwanamke raia wa Uganda anayedaiwa kumdunga kisu mara kadhaa na kumuua mke-mwenza katika kitongoji duni cha Mathare, jijini Nairobi.

Sarah Namono anazuiliwa katika Kituo cha Polisi cha Pangani.

DCI ilisema mauaji ya Bi Grace Kibone yalitekelezwa mnamo Ijumaa, Septemba 23.

Tukio hilo liliripotiwa na mfanyakazi wa hospitali pamoja na jamaa wa mwendazake.

Mhasiriwa aliyekuwa anavuja damu vibaya alikimbizwa katika kliniki ya Médecins Sans Frontières (MSF) kwenye barabara ya Juja Road ambapo alitangazwa kwamba amekufa.

Kwingineko, katika eneo la Njiru, jijini Nairobi, polisi wanamzuilia mwanamke aliyedaiwa kumchoma kwa maji moto mwanamke na mtoto wake kwa tuhuma kwamba alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na mume wake.

Mercy Moraa anazuiliwa katika kituo cha Polisi cha Obama ambapo uchunguzi unaendelea kuhusu shambulizi hilo lililowasababishia majeraha mwilini wahasiriwa hao wawili.

“Mshtakiwa (Moraa) alitekeleza hatia hiyo ya kumchoma kwa maji moto mwanamke (jina lake limebanwa) mwenye umri wa miaka 25 na mtoto wa kike (jina limebanwa) mwenye umri wa miaka mitatu baada ya kushuku kuwa mhasiriwa alikuwa na uhusiano wa kimapenzi na bwanake,” alisema Konstebo wa Polisi Amos Ouko.

  • Tags

You can share this post!

MITAMBO: Kifaa cha kubaini ubora wa udongo kuwafaa wakulima

Zetech Sparks yasajili watano

T L