Raia waadhimisha miaka 10 ya kung’oa utawala wa Gaddafi

Raia waadhimisha miaka 10 ya kung’oa utawala wa Gaddafi

Na AFP

RAIA wa Libya mnamo Jumatano waliadhimisha miaka 10 tangu utawala wa kiimla wa aliyekuwa Rais wa nchi hiyo, Muammar Gaddafi, uondolewe mamlakani kutokana na maandamano makubwa.

Tangu kung’olewa kwa marehemu Gaddafi, Libya imekuwa ikikumbwa na misukosuko ya kisiasa kutokana makundi mawili pinzani yanayozozania uongozi.

Wananchi wenye furaha walijazana barabarani Magharibi mwa Libya ili kutazama magwaride ya wanajeshi na kufuatilia hotuba mbalimbali huku baruti zikilipuliwa na wengi kushangilia.

“Watu wamefurahi na hatujutii kamwe. Nina matumaini kwamba nchi yetu itapata amani siku moja,” akasema Ziad Arabi jijini Tripoli.

Kaimu Waziri Mkuu Hamid Dbeibah naye aliungana na raia kufurahia maadhimisho hayo huku akitembea jijini Tripoli akiwa chini ya ulinzi mkali.

 

You can share this post!

WANDERI KAMAU: Tujinasue sasa kutoka kwa mfumo wa kibepari

Ruto akubaliana na Raila kuwa kaulimbiu ya...