Raila asema amepata mbinu kuteka Mlima

Raila asema amepata mbinu kuteka Mlima

GEORGE ODIWOUR na BENSON MATHEKA

KIONGOZI wa chama cha ODM, Raila Odinga, ameambia wafuasi wake wa Nyanza kwamba, hatimaye amegundua siri ya kupenya eneo la Mlima Kenya ambalo limekuwa likimnyima nafasi ya kushinda uchaguzi wa urais.

Akizungumza katika Kaunti ya Homa Bay alikohudhuria mazishi ya David Ajwang Nyakwamba, baba ya seneta wa kaunti hiyo, Moses Kajwang na mbunge wa Ruaraka TJ Kajwang, Bw Odinga alisema amegundua njia ya kushinda kura katika eneo hilo.

“Wakati huu nimeona barabara ya kuingia Mlima Kenya. Nimetambua jinsi ninavyoweza kupenya eneo la kati ya nchi na hakuna kurudi nyuma,” alisema.

Bw Odinga anayejiandaa kugombea urais kwa mara ya tano, anachukuliwa kuwa chaguo la Rais Uhuru Kenyatta kumrithi kwenye uchaguzi mkuu wa 2022.

Kwa muda wa miaka mitatu sasa, amekuwa akishirikiana kwa karibu na Rais Kenyatta ambaye ametofautiana vikali na Naibu Wake William Ruto.

You can share this post!

Wezi wa parachichi wasakwa Kakuzi

Ndugu waliouawa na polisi wazikwa wengine wanne wakiuawa...