Raila ataja sera atakayofuata akiibuka mshindi mwaka 2022

Raila ataja sera atakayofuata akiibuka mshindi mwaka 2022

Na JUSTUS OCHIENG

KIONGOZI wa ODM, Bw Raila Odinga amependekeza kuwa wafanyakazi wazembe wa umma hawafai kupandishwa vyeo, kuongezwa ujira kwani ni mzigo kwa serikali.

Katika kile kilichoonekana kama ruwaza yake kuhusu utumishi wa umma unaohitajika nchini, Bw Odinga pia alipendekeza kuwa wafanya wasiojitolea kazini wanafaa kufutwa badala ya kuendelea kulipwa mishahara.

Hii ni sehemu ya msururu wa mwongozo ambao anatarajia kutekeleza nchini endapo atachaguliwa kuwa Rais katika uchaguzi mkuu ujao.

“Taifa hili linapaswa kuwa na mfumo maalum wa kuhakikisha kuwa wafanyakazi wa umma wanalipwa mishahara na marupurupu kulingana na utendakazi wao ili sekta hiyo ivutie wafanyakazi wengi wenye ujuzi mkubwa,” Bw Odinga akasema kwenye taarifa.

Akaongeza: “Hii ndiyo njia ya kipekee ya kuhakikisha wanauma na wanawake wenye ujuzi mkubwa wanajiunga na utumishi wa umma. Baada ya hapo, tunaweza kufanya ukadiriaji wa utendakazi wa sekta ya umma kwa kuwahakikisha wafanyakazi wote wanatia saini mkataba wa utendakazi.”

You can share this post!

Wafanyakazi walioangukia ‘manna’ waamrishwa wairejeshe

Japan wapepeta Mexico na kuendeleza ubabe wao kwenye...