Siasa

Raila azuru Kilifi kukipa chama cha ODM mvuto mpya

January 24th, 2024 1 min read

NA ALEX KALAMA

KIONGOZI wa chama cha Orange Democratic Movement (ODM) Raila Odinga amewasili katika ukumbi wa Red Cross mjini Malindi, Jumatano asubuhi kwa ajili ya kuzindua rasmi shughuli ya kuwasajili wanachama katika Kaunti ya Kilifi.

Ziara yake inalenga kukipa chama cha ODM mvuto mpya.

Bw Odinga ameandamana na Seneta wa Nairobi Edwin Sifuna na aliyekuwa Gavana wa Kakamega Wycliffe Oparanya ambaye pia ni Naibu Kiongozi wa ODM.

Pia viongozi wa Kilifi wakiongozwa na Gavana Gideon Mung’aro, Seneta wa Kilifi Steward Madzayo, mbunge wa Malindi Amina Mnyazi, mbunge wa Magarini Harry Kombe na Spika wa Bunge la Kilifi Teddy Mwambire wamekuwepo kumpa Bw Odinga makaribisho.

Kwenye ziara hiyo pia yupo Gavana wa Mombasa Abdulswamad Sharrif Nassir ambaye wakati wa makumbusho ya aliyekuwa makamu wa rais wa kwanza nchini, marehemu Jaramogi Oginga Odinga, aliahidi kuita barabara mojawapo jijini Mombasa jina la babake kiongozi wa ODM.

Akitoka katika ukumbi wa Red Cross, Bw Odinga ataelekea kwa uwanja wa chuo cha kiufundi cha Marafa Polytechnic katika wadi ya Marafa iliyoko eneobunge la Magarini ambapo hapo ndipo kutakuwa kilele cha mkutano huo.

Tunaandaa habari kamili…