Raila kifua mbele kura ya maoni ya TIFA

Raila kifua mbele kura ya maoni ya TIFA

NA CHARLES WASONGA

MWANIAJI urais wa muungano wa Azimio la Umoja-One Kenya Raila Odinga imempiku kwa umaarufu mwaniaji wa urais wa muungano wa Kenya Kwanza William Ruto.

Hii ni kulingana na matokeo ya kura ya maoni yaliyotolewa Jumatano, Mei 18, 2022, na kampuni ya utafiti ya TIFA.

Bw Odinga ana umaarufu wa asilimia 39 huku Ruto akiwa na umaarufu wa asilimia 35, kulingana na utafiti huo ulioendeshwa mnamo Jumatatu, Mei 16, 2022 baada ya wawili hao kuwateua wagombea wenza wao.

Naye kiongozi wa Wiper Kalonzo Musyoka alipata umaarufu wa asilimia mbili huku wagombeaji wengine wa urais wakipata chini ya asilimia moja ya kura.

Bw Odinga alimteua kiongozi wa Narc Kenya Martha Karua kuwa mgombea mwenza wake huku Dkt Ruto akimteua Mbunge wa Mathira Rigathi Gachagua.

Naye Bw Musyoka alimteua aliyekuwa mwaniaji wa kiti cha ugavana Narok Andrew Sunkuli kuwa mgombea mwenza wake.

Utafiti huo ulibaini kuwa asilimia 14 ya wapiga kura bado hawajaamua mgombea urais ambaye watampigia kura.

  • Tags

You can share this post!

Mazao yanayonawiri maeneo kame yana mchango mkubwa...

Vishale: Maafande wa Nakuru Mashariki ndio mabingwa wa taji...

T L