Raila kuvumisha Azimio mjini Thika mnamo Jumamosi

Raila kuvumisha Azimio mjini Thika mnamo Jumamosi

Na CHARLES WASONGA

KIONGOZI wa ODM Raila Odinga, Jumamosi atafanya mkutano wa kampeni mjini Thika, Kaunti ya Kiambu.

Akiongea na vijana kutoka eneo la Mlima Kenya katika afisi za Wakfu wa Jaramogi Oginga, Jumanne Januari 11, 2022, Bw Odinga alisema atafafanua ajenda yake kwa wakazi wa eneo hilo.

“Mnamo Jumamosi tutawasili Thika. Huo ndio utakuwa mkutano wetu wa kwanza wa kutangamana na wakazi wa eneo la Mlima Kenya tangu kuanza kwa mwaka huu,” Bw Odinga akasema.

Kiongozi huyo wa ODM alisema mkutano huo ambao utafanyika katika uwanja wa michezo wa Thika, utampa nafasi ya kuuza sera za Azimio la Umoja kwa wakazi.

Tangu Januari 1, 2022, Bw Odinga hajafanya mikutano ya hadhara, isipokuwa hafla za mazishi katika kaunti za Nakuru na Kajiado.

Kaunti za Kiambu na Murang’a ni ngome za kisiasa za Rais Uhuru Kenyatta, kiongozi wa Jubilee.

  • Tags

You can share this post!

Maseneta kuendesha vikao vya kukusanya maoni kuhusu mswada...

Okutoyi aanza mazoezi nchini Australia baada ya vipimo...

T L