Raila Odinga amteua Martha Karua awe mgombea mwenza wake

Raila Odinga amteua Martha Karua awe mgombea mwenza wake

NA MWANDISHI WETU

KIONGOZI wa ODM ndani ya Azimio La Umoja┬áRaila Odinga amemteua kiongozi wa Narc-Kenya Martha Karua awe mgombea mwenza wake katika kinyang’anyiro cha urais Agosti 9, 2022.

Akizungumza katika Ukumbi wa Kimataifa wa Kenyatta jijini Nairobi (KICC), Raila amemtaja Karua kama mtu mwenye rekodi thabiti ya kutetea haki za binadamu.

“Nilimtaka mtu mkakamavu na baada ya kupiga darubini na kufanya mashauriano ya kina, nimeamua huyu mtu awe ni mwanamke,” Raila amesema.

Bi Karua amekubali wajibu aliotwikwa na mgombea wake mkuu na vile vile akapongeza jopo lililosimamia mchakato mzima.

“Ninapongeza jopo la Azimio la Umoja kwa kuendesha shughuli muhimu kwa uwazi hadi mwishowe akapatikana mgombea mwenza. Ninawapongeza wenzangu waliomezea mate nafasi hii,” amesema Bi Karua.

  • Tags

You can share this post!

PAUKWA: Bikizee akumbana na kudura ya Mungu

TALANTA YANGU: Matunda ya mfumo wa CBC

T L