Habari MsetoSiasa

Raila Odinga Junior aitaka serikali ihalalishe bangi

September 14th, 2018 1 min read

NA MWANDISHI WETU

MWANAWE aliyekuwa Waziri Mkuu Raila Odinga, Raila Junior ameitaka serikali kuwazia kuhalalisha matumizi ya bangi, ili kusaidia wafanyabiashara wa dawa hiyo ya kulevya ama watu wa dini wanaoitumia katika shughuli zao.

Raila Junior anasema kuna haja ya serikali kuangazia suala hilo kwa umuhimu na kwa haraka.

Mnamo 2015, Mbunge wa Kibra Ken Okoth aliwataka wakulima wa miwa kutoka magharibi mwa Kenya wakuze bangi badala ya zao hilo ambalo haliwaletei faida.

Mnamo 2016, Bw mtafiti Sammy Gwada Ogot aliwasilisha ombi katika seneti akitaka bangi ihalalishwe kwa misingi hiyo ya kuwa na uwezo wa kutibu magonjwa.