Rais akamatwa

Rais akamatwa

Na RICHARD MUNGUTI

RAIS wa Shirikisho la Kandanda Nchini (FKF) alikamatwa muda mfupi baada ya Mahakama kuu ya Milimani kukataa kusitisha kuteuliwa kwa kamati ya kusimamia kambumbu na Waziri wa Michezo Amina Mohamed Ijumaa alasiri

Mwendwa alikamatwa na maafisa kutoka idara ya uchunguzi wa jinai (DCI). Alipelekwa kuzuiliwa katika makao makuu ya DCI. Msemaji wa Polisi Bruno Shioso alithibitisha kukamatwa kwa Mwendwa. FKF, Mwendwa na kinara wa shirikisho la kandanda Barry Otieno waliwasilisha kesi ya dharura wakiomba kamati inayoongozwa na Jaji (mstaafu) Aaron Ringera ikianza kutekeleza majukumu yake.

Akikataa kupiga kalamu kamati hiyo Jaji Hedwing Ong’udi, alisema harakati za kuzindua utenda kazi wa kamati hiyo ulianza Oktoba 14, 2021. “Kamati ya Ringera ilianza kazi Oktoba 14 2021 na wale ambao hawakuridhika wangelishtaki wakati huo.Sasa siwezi kusitisha utendakazi wake,” Jaji Ong’undi aliamuru.

Jaji huyo aliagiza hiyo isikizwe Novemba 23, 2021. Katika kesi hiyo FKF imewashtaki  Bi Mohamed, Msajili wa masuala ya Michezo, Kamati ya Usimamizi wa FKF na Mwanasheria mkuu.

Wakili Charles Njenga anayewakilisha FKF , Mwendwa na Otieno aliomba mahakama kuu isitishe utenda kazi wa kamati hiyo ya Ringera , akidai Waziri alikaidi sheria alipoiteua. Bw Njenga alieleza mahakama uteuzi wa kamati hiyo itakayomulika ubadhirifu wa pesa unakinzana na Katiba na sheria za usimamizi wa dimba nchini.

 

You can share this post!

PETER NGARE: Wakenya waache kasumba ya ‘Mtu...

JUMA NAMLOLA: Bunge lisitumiwe kama ‘danganya...

T L