Rais amteua mrithi wa mkuu wa majeshi Jenerali Samson Mwathethe

Rais amteua mrithi wa mkuu wa majeshi Jenerali Samson Mwathethe

Na NYAMBEGA GISESA

RAIS Uhuru Kenyatta amempandisha cheo Luteni Jenerali Robert Kibochi awe Jenerali na kumfanya Mkuu wa Majeshi kurithi nafasi ya Samson Mwathethe anayestaafu.

Kibochi ataanza kazi rasmi kusimamia wanajeshi Mei 11.

Hatua hii imechukuliwa na kiongozi wa nchi kwa sababu Mwathethe anastaafu.

Jenerali Mwathethe alikuwa ni mwanajeshi wa pili kutoka kikosi cha wanamaji kuwa Mkuu wa Majeshi.

Wa kwanza alikuwa Jenerali Joseph Kibwana.

You can share this post!

Anayetakiwa Afrika Kusini kwa utekaji nyara aachiliwa huru

Mmiliki nyumba ang’oa paa, avunja milango akidai kodi

adminleo