Habari

Rais Kenyatta atarajiwa kufungua rasmi maonyesho ya kimataifa ya Mombasa

September 5th, 2019 1 min read

Na CHARLES WASONGA

RAIS Uhuru Kenyatta anatarajiwa leo Alhamisi kujiunga na maelfu ya Wakenya, wafanyabiashara wa nchi za kigeni na wafanyabiashara wa kuwasilisha bidhaa na huduma kwenye Maonyesho ya Kilimo katika uwanja wa Maonyesho wa Jomo Kenyatta ulioko Mkomani jijini Mombasa kwa ufunguzi rasmi wa Maonyesho ya Kimataifa ya Mombasa ya mwaka 2019.

Wakati wa ufunguzi rasmi wa maonyesho hayo, Rais ambaye ni mdhamini wa Shirika la Maonyesho ya Kilimo nchini (ASK) atazuru vibanda kadhaa vya maonyesho, kutoa hotuba rasmi na pia kuwatunuku waonyeshaji bidhaa na huduma watakaotia fora katika maonyesho hayo.

Maonyesho ya Kimataifa ya Mombasa ya mwaka 2019 ambayo yalianza Jumatano, Septemba 4, 2019, yamevutia zaidi ya wafanyabiashara 190 wa bidhaa na huduma kutoka mataifa ya Uganda, Tanzania, Ukraine, China na Visiwani Zanzibar