Michezo

Rais Mnangagwa awataka raia waifae timu ya taifa kwa hali na mali

June 15th, 2019 1 min read

Na MASHIRIKA

HARARE, Zimbabwe

RAIS Emmerson Mnangagwa amewataka raia wa taifa hili waisaidie timu ya taifa kwa hali na mali, huku akiwakumbusha kwamba ufanisi wa timu hiyo ni ufanisi wa taifa kwa jumla.

“Tunawaunga mkono wanasoka wetu kwa sababu hakuna sababu ya kukosa kuwaunga mkono. Sisi ni Warriors na wao ni Warriors vilevile, sisi ni Wazimbabwe na wao pia ni Wazimbabwe,” aliongeza Rais huyo.

Mnangagwa alisema, Warriors watakapokuwa wakishiriki michuano ya AFCON watakuwa huko kama mabalozi wa nchi nzima kwa vile watakuwa na nembo ya taifa kwenye mavazi yao.

“Tutaendelea kuchangisha fedha kwa ajili ya kikosi chetu, na mchango wetu unapaswa kuleta mafanikio kupitia kwa Nyanja za michezo. Nawaomba wadau wote waunge mkono timu ya taifa,” alisema Rais Mnangagwa.

 

Imekusanywa na John Ashihundu