Habari za Kitaifa

Rais Ruto ataka mswada upitishwe upesi ili ‘vijana wapate kazi’

Na MANASE OTSIALO June 20th, 2024 1 min read

RAIS William Ruto ameambia wabunge wapitishe Mswada wa Fedha 2024 akisema utasaidia walimu wa JSS kupata kazi, pamoja na vijana kupata mikopo ya elimu ya juu.

Akizungumza katika Kaunti ya Garissa baada ya kuhudhuria hafla ya kufuzu katika Chuo Kikuu cha Garissa Alhamisi, Dkt Ruto alisema mswada huo utasaidia miradi mingi ikiwemo kufanikisha lishe kwa watoto shuleni, barabara pamoja na shughuli zingine muhimu nchini.

Rais amesema hayo wakati ambapo maandamano yamechacha katika sehemu mbali mbali nchini, ikiwemo katika ngome zake za Eldoret, Nakuru, Nyeri kuhusu mswada huo waandamanaji wakitaka upigwe chini.

Waandamanaji ambao wengi wao ni chipukizi wa Gen Z wameutaja mswada huo kuwa dhalimu, wakisema unawakandamiza kiuchumi wakilaumu Serikali kwa kutosikia kilio chao.

Wabunge wanajadili mswada huo tatanishi na kura inatarajiwa kupigwa baadaye jioni kuona wapo utapita au la.