Habari Mseto

Rais wa Honduras na mkewe wapatikana na corona

June 17th, 2020 1 min read

NA AFP

Rais wa Hounduras amesema kwamba yeye na mke wake wamepatikana na virusi vya corona.

Nchi hiyo ya Amerika ya Latini ina visa chini ya 10,000 vya virusi hivyo kulingana na Wizara ya Afya, na vifo 330.

“Wikendi nilianza kujihisi vibaya na leo nimepimwa na nikapatikana na virusi vya corona,” alisema Juan Orland Hernandez alipohutubia nchi Jumatano.

Rais huyo mwenye miaka 51 alisema kwamba atafanya kazi kupitia mitandao huku akipokea matibabu.

Tangu mwanzoni mwa janga la corona Mach, Hernandez amekuwa katika mstari wa mbele kukabiliana na virusi vya corona.

Katika hatuba nyingi alizotoa, amesisitiza wananchi wanafaaa kuosha mikono, kuvaa barakoa na kujitenga na wengine.

Hata baada ya kuweka kafyu bado virusi hivyo vinaendelea kusambaa na kuongezeka huku polisi wakihakikisha kwamba watu wamekaa nyumbani nchini humo.