Kimataifa

Rais wa pili wa Tanzania Ali Hassan Mwinyi aaga dunia

February 29th, 2024 1 min read

NA THE CITIZEN, Tanzania

Rais wa pili wa Tanzania Ali Hassan Mwinyi ameaga dunia.

Kulingana na taarifa kutoka Ikulu ya Dodoma na Rais Samia Suluhu Hassan, Februari 29, 2024, Mzee Mwinyi ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 98.

Soma pia Watanzania walalamika sanamu iliyozinduliwa Ethiopia si sura ya Nyerere!

Mwinyi alikuwa Rais wa Pili baada ya Julius Nyerere kuondoka mamlakani, na alihudumu kati ya 1985-1995.

Amefariki miezi mitatu tu kabla aadhimishe miaka 99 ya kuzaliwa kwake.

Mnamo Februari 24, alikimbizwa hospitalini akiugua maradhi ya kifua.

Soma pia: Tanzania yapata treni za umeme, Kenya ikisukuma maisha na za kizamani

Kisha: Wakenya ni miongoni mwa 25 waliofariki katika ajali Tanzania