Rais wa Tanzania John Magufuli afariki

Rais wa Tanzania John Magufuli afariki

NA AGGREY MUTAMBO

RAIS wa Jamhuri ya Tanzania John Pombe Magufuli amefariki. Kulingana na tangazo la Makamu wa Rais Bi Samia Suluhu kwenye runinga, Bw Magufuli, aliye na miaka 61, alifariki kutokana na mshtuko wa moyo.  

Aliambia wananchi wa taifa hilo kuwa rais huyo alifariki Jumatano jioni baada ya kukimbizwa katika hospitali moja jijini Dar es Salaam mnamo Machi 6, 2021, ambapo amekuwa akihudumiwa na madaktari wa mpigo wa damu.

“Kwa huzuni kuu, tunatangaza kuwa leo, Mchi 17, saa kumi na mbili jioni, tulimpoteza kiongozi wetu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Joseph Magufuli kutokana na matatizo ya moyo katika Hospitali ya Muzena hapa Dar es Salaam. Mipango ya mazishi inaendelea. Taifa letu litamwomoleza kwa siku 14 na bendera zetu zitapandishwa nusu mlingoti,” alisema Bi Suluhu.

Kifo chake kimefikisha kikomo wiki za masuali mengi kuhusu alipo rais wa Tanzania na afya yake., wengi wakidai mitandaoni kuwa alikuwa anaugua virusi vya corona. Hata hivyo, pia kinafungua ukurasa mpya kwa taifa ambalo halijawahi kubadilisha uongozi wa urais nje ya uchaguzi mkuu.

Kulingana na Katiba ya Tanzania, Makamu wa Rais anafaa kuchukua hatamu za uongozi kwa kipindi kilichosalia cha Rais Magufuli. Akiwa tu na miezi mitano katika muhula wa pili wa uongozi, inamaanisha Makamu wa Rais Samia Suluhu atakuwa rais wa kwanza mwanamke wa Tanzania na hata katika Jumuia ya Afrika Mashariki.

Bw Magufuli, aliyejulikana kw ajina la utani ‘The Bulldozer’ kwa kutekeleza miradi mingi wakati akiwa Waziri wa Barabara na Ujenzi, hajaonekana hadharani tangu Februari 27, na kuzua uvumi kuwa huenda amegonjeka.

Akiwa mkosoaji mkuu wa janga la corona, Bw Magufuli alidinda kufunga nchi yake wakati mataifa jirani yalifanya hivyo kuzuia kusambaa kwa virusi vya corona. Pia, alishangaza dunia kwa kukosa kuwaagiza Watanzania kuvaa maski kwenye mikutano ya umma. Badala yake, aliwasihi wananchi kumuomba Mola airehemu Tanzania.

 

You can share this post!

Serikali yasema itaondoa barabarani matatu zionazokaidi...

MAFUTA: Wakenya wakimbilia Tanzania