Kimataifa

Rais wa Tunisia afariki akiwa na umri wa miaka 92

July 25th, 2019 1 min read

Na MASHIRIKA

TUNIS, TUNISIA

RAIS wa Tunisia, Beji Caid Essebsi amefariki katika hospitali ya kijeshi jijini Tunis, imetangaza asasi ya urais nchini humo.

Essebsi ameaga dunia saa nne na dakika ishirini na tano asubuhi (10:25 am) saa za eneo hilo la Afrika Kaskazini mapema Alhamisi.

Alilazwa hospitalini Jumatano, ikiwa mara ya pili katika kipindi cha mwezi mmoja.

Essebs aliyekumbana na mauti akiwa na umri wa miaka 92 amekuwa uongozini tangu mwaka 2014.

Aidha, amekuwa ni mmojawapo wa wakuu wa mataifa yao wenye umri wa juu zaidi.