Rais wa UAE Khalifa bin Zayed Al Nahyan afariki

Rais wa UAE Khalifa bin Zayed Al Nahyan afariki

NA MASHIRIKA

ABU DHABI, UAE

RAIS wa Miliki ya Uarabuni (UAE) Khalifa bin Zayed Al Nahyan amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 73.

“Wizara ya masuala ya rais, inaomboleza pamoja na watu wa UAE na dunia nzima. Kiongozi wetu Sheikh Khalifa bin Zayed Al Nahyan, Rais wa Nchi alifariki pembeni mwa Mungu leo,” shirika la habari la serikali, WAM, lilitangaza.

Serikali ilitangaza siku 40 za maombolezo kuanzia leo Jumamosi. Ofisi za serikali na mashirika ya kibinafsi hazitafunguliwa kwa siku tatu.

Sheikh Khalifa hajakuwa akitekeleza majukumu yake tangu 2014 alipokumbwa na ugonjwa kiharusi.

Ndugu yake Sheikh Mohammed bin Zayed, ndiye amekuwa akiendesha shughuli za serikali na sasa atatawazwa rasmi kuchukua hatamu za uongozi.

Sheikh Khalifa aliteuliwa kuwa rais wa UAE mnamo 2004, kutoka kwa baba yake, Sheikh Zayed al Nahyan.

Kabla ya kuteuliwa kuwa rais, Sheikh Khalifa, alikuwa mwanamfalme aliyesimamia Abu Dhabi na aliongoza Baraza Kuu la Petroli la Abu Dhabi ambalo hutengeneza sera za mafuta.

You can share this post!

Mkataba wa Musalia, Ruto watatiza Mlima

Mtandao wa BrighterMonday wapendelewa zaidi na watafutaji...

T L