Rais wa zamani wa LSK ataka mtaalam wa maabara kortini

Rais wa zamani wa LSK ataka mtaalam wa maabara kortini

Na RICHARD MUNGUTI

ALIYEKUWA rais wa chama cha mawakili nchini (LSK) anataka mtaalamu wa maabara ya serikali afike kortini kutoa ushahidi na ripoti aliyotayarisha ya dawa za kulevya zilizopatikana na mwanablogi.

Bw Erick Mutua anayemwakilisha Hegman Osotshi Speke alipinga vikali ripoti ya dawa za kulevya iliyotayarishwa na Bi Eunice Wambugu Njugu ikitolewa kama ushahidi mahakamani na afisa mwingine.

Bw Mutua alisema ni kinyume cha sheria kwa ripoti ya dawa za kulevya zinazodaiwa kupatikana kwa Bw Speke ikitolewa mahakamani na afisa ambaye hakuiandaa. Bw Mutua alisema makosa ambayo Speke alifanya ni kuchapisha habari za kumdunisha Rais Uhuru Kenyatta.

katika mitandao ya kijamii na wala sio kupatikana na dawa za kulevya aina ya heroin gramu 16.31 zenye thamani ya Sh48,930. Hakimu mwandamizi Bi Martha Nanzushi atatoa uamuzi Desemba 6,2021 ikiwa ataamuru Bi Njugu, anayesemekana amestaafu afike kortini.

You can share this post!

Real Madrid wakung’uta Granada na kurejea kileleni...

Utakosa huduma za serikali na mikahawani ikiwa haujapata...

T L