Habari Mseto

Rais wa zamani wa Mali afariki

September 21st, 2020 1 min read

AFP

Aliyekuwa Rais wa Mali Moussa Traore aliyeiongoza Mali kutoka 1968 mpaka alipotolewa mamlakani na mapinduzi mwaka 1991 alifariki nyumbani kwake katika jiji kuu la Bamako, familia yake ilisema.

Alifariki Jumanne akiwa na umri wa miaka 83. “Tunauomboleza,” binamuye Mohamed Traore alisema.

Moussa Traore ambaye kwa wakati huo alikuwa Luteni ndiye aliyeongoza mapinduzi hayo yaliomtoa mamlakani Modibo Keita rais wa kwanza baada ya kupata ya kupata uhuru 1968.

TAFSIRI na FAUSTINE NGILA