Michezo

Rami afichua alikuwa akimumunya mwanamitindo mkongwe

June 25th, 2020 2 min read

Na CHRIS ADUNGO

BEKI fumbwe mzawa wa Ufaransa ambaye kwa sasa huvalia jezi za kikosi cha PFC Sochi nchini Urusi, Adil Rami, 34, amepasua mbarika kuhusu jinsi alivyo kidume katika masuala ya chumbani.

Kupitia ufichuzi wa mwanasoka mwenzake kambini mwa Sochi, Rami alikuwa akishiriki miereka ya siri chumbani wakati alipokuwa akitoka kimapenzi na mwigizaji mkongwe mzawa wa Canada, Pamela Anderson, 52, kwa hadi mara 12 kwa usiku mmoja.

Nyota huyo wa zamani wa AC Milan ya Italia na Olympique Marseille ya Ufaransa, aliwahi kutikisa buyu la asali la Anderson kwa kipindi cha miaka miwili kabla ya kutemwa na mwanamitindo huyo raia wa Amerika mnamo 2019 kwa madai ya kuwa na jicho kali la nje.

Hadi Rami alipotemwa na Pamela kama ‘Big-G’, wawili hao walioanza kuhusiana mnamo 2017, walikuwa wakiishi pamoja katika kasri la kidosho huyo katika eneo la Cassis viungani mwa mji wa Marseile.

Kabla ya kuanza kumtambalia Pamela kimapenzi, Rami alikuwa katika uhusiano mwingine na kichuna Sidonie Biemont aliyemzalia pacha wa kiume, Zayn na Madi mnamo 2016.

Rami aliingia katika sajili rasmi ya Sochi mwanzoni mwa mwaka huu na mchezaji mwenzake, Aleksandr Kokorin, amefichua kwamba mwanasoka huyo wa zamani wa Valencia na Sevilla, alikuwa akijigamba sana kuhusu mahusiano yake ya kimapenzi na ukali wake katika michezo ya chumbani isiyohitaji refa.

“Rami alituhadithia mambo mengi matamu kumhusu Pamela, nasi tukatamani sana kujua jinsi uhusiano wao ulivyokuwa chumbani. Alikuwa akimsifu mara kwa mara akidai hakuna demu anayemzidi kichuna huyo kwa ufundi wa kucheza ngoma za siri,” akasema Kokorin, 29, katika mahojiano yake na gazeti la Marca, Urusi.

“Alisema yeye na Pamela wangalipigana miereka kwa hadi mara 12 kila usiku bila kuchoka,” akaongeza katika kauli iliyoungwa na mchezaji mwenzao, Oleksandr Aliyev.

Pindi baada ya Kokorin kufichua hayo, Pamela aliandika kwenye mtandao wake wa Instagram: “Aliyoyasema Rami kwa wenzake kambini mwa Sochi ni ya kweli. Angalikuwa bado analitomasa tunda hili atakavyo iwapo angaliridhika nalo. Jicho la nje lilimponza. Lakini ustadi wake chumbani ulimfanya mzembe uwanjani, akaanza kupata majeraha ya mara kwa mara yaliyotishia kumvurugia taaluma ya soka.”