Michezo

Ratiba ya Ligi Kuu ya Kenya msimu 2019-2020 yatangazwa

June 21st, 2019 6 min read

Na GEOFFREY ANENE

LIGI Kuu ya Soka ya Kenya ya msimu 2019-2020 itaanza Agosti 30, 2019, na kutamatika Mei 17, 2019, kampuni inayoendesha ligi hiyo ya klabu 18 imetangaza Ijumaa.

Mabingwa mara 18 Gor Mahia wataanza kutetea ubingwa wao dhidi ya washindi mara 11 Tusker hapo Septemba 1.

Gozi maarufu kati ya Gor na mahasimu wao wa tangu jadi AFC Leopards, ambalo linafahamika kwa jina la utani kama ‘Mashemeji Derby’ litasakatwa Novemba 10 na Machi 15 uwanjani Kasarani.

Viwanja vitakavyotumika msimu huu ni Kasarani (Nairobi), Nyayo (Nairobi), Kenyatta (Machakos), Moi (Kisumu), Green Stadium (Awendo), Bukhungu (Kakamega), Sudi (Bungoma), Mbaraki (Mombasa), Green Stadium (Kericho), Ruaraka (Nairobi), Afraha (Nakuru), Mumias Sports Complex (Kakamega) na Chemelil Sports Complex (Chemelil).

Nyayo haujatumiwa kwa muda mrefu.

Uwanja wa Nyayo, Nairobi. Picha/ Hisani

Ulifungwa mapema mwaka 2017 kufanyiwa ukarabati. Tangu wakati huo, umetumika kwa sherehe za Jamhuri Dei mwaka 2018 na mbio za kilomita 21 za First Lady Half Marathon mwezi Machi 2019. Mechi kati ya KCB na Bandari imeratibiwa kusakatiwa uwanjani Nyayo hapo Machi 8, 2020.

Msimu huu bado utashuhudia timu 18 zikiwania ubingwa unaondamana na tiketi ya kushiriki mashindano ya kifahari ya Klabu Bingwa Afrika.

Timu hizi ni AFC Leopards, Bandari, Chemelil Sugar, Kakamega Homeboyz, Kariobangi Sharks, KCB, Mathare United, Nzoia Sugar, Sofapaka, SoNy Sugar, Tusker, Ulinzi Stars, Western Stima na Zoo.

Wazito imerejea Ligi Kuu baada ya msimu mmoja kwenye Ligi ya Daraja ya Pili (Ligi ya Supa). Ilifuzu moja kwa moja pamoja na Kisumu All Stars kwa kumaliza ligi hiyo katika nafasi mbili za kwanza msimu 2018-2019.

Posta Rangers, ambayo ililemea Nairobi Stima katika mechi ya kupandishwa/kuteremshwa kwenye Ligi Kuu kwa jumla ya mabao 3-2 siku chache zilizopita, inakamilisha orodha ya washiriki 18.

Kwa kawaida, Ligi Kuu imekuwa ikishuhudia timu mbili za mwisho zikitemwa moja kwa moja, huku nambari 16 ikimenyana na nambari tatu kutoka Ligi ya Supa kuamua mshiriki wa Ligi Kuu msimu unaofuata.

Vihiga United na Mount Kenya zilishushwa ngazi hadi Ligi ya Supa kwa kutamatisha Ligi Kuu katika nafasi mbili za mwisho. Rangers ililazimika kujihakikishia msimu mwingine kwenye Ligi Kuu kwa kulemea Nairobi Stima iliyomaliza Ligi ya Supa katika nafasi ya tatu.

Ratiba ya Ligi Kuu ya Kenya (msimu 2019-2020):

Agosti 30, 2019

3:00 PM Kariobangi Sharks na Western Stima (Kasarani)

Agosti 31, 2019

2:00 PM Wazito na Nzoia Sugar (Machakos)

3:00 PM Kisumu All Stars na Ulinzi Stars (Moi Stadium, Kisumu)

3:00 PM Mathare United na Bandari (Kasarani)

3:00 PM SoNy Sugar na KCB (Green Stadium, Awendo)

4:15 PM Sofapaka na Posta Rangers (Machakos)

Septemba 1, 2019

3:00 PM Gor Mahia na Tusker (Machakos)

3:00 PM Kakamega Homeboyz na AFC Leopards (Bukhungu)

3:00 PM Zoo na Chemelil Sugar (Kericho Green)

Septemba 14, 2019

3:00 PM Bandari na Zoo (Mbaraki)

3:00 PM Chemelil Sugar na Gor Mahia (Moi Stadium, Kisumu)

3:00 PM KCB na Kisumu All Stars (Machakos)

3:00 PM Nzoia Sugar na SoNy Sugar (Sudi Stadium, Bungoma)

3:00 PM Tusker na Mathare United (Ruaraka)

3:00 PM Ulinzi Stars na Sofapaka (Afraha)

3:00 PM Western Stima na Wazito (Moi Stadium, Kisumu)

Septemba 15, 2019

2:00 PM Posta Rangers na Kakamega Homeboyz (Machakos)

4:15 PM AFC Leopards na Kariobangi Sharks (Machakos)

Septemba 21, 2019

2:00 PM Posta Rangers na Western Stima (Machakos)

3:00 PM Kisumu All Stars na Nzoia Sugar (Moi Stadium, Kisumu)

3:00 PM Mathare United na Ulinzi Stars (Kasarani)

3:00 PM SoNy Sugar na Bandari (Green Stadium, Awendo)

4:15 PM Wazito na AFC Leopards (Machakos)

Septemba 22, 2019

2:00 PM Sofapaka na Chemelil Sugar (Machakos)

3:00 PM Kakamega Homeboyz na Kariobangi Sharks (Bukhungu)

3:00 PM Zoo na Tusker (Kericho Green)

4:15 PM Gor Mahia na KCB (Machakos)

Septemba 28, 2019

3:00 PM Bandari na Posta Rangers (Mbaraki)

3:00 PM Kariobangi Sharks na Mathare United (Kasarani)

3:00 PM KCB na Kakamega Homeboyz (Machakos)

3:00 PM Kisumu All Stars na Western Stima (Moi Stadium, Kisumu)

3:00 PM Nzoia Sugar na Gor Mahia (Mumias Sports Complex)

3:00 PM Ulinzi Stars na SoNy Sugar (Afraha)

Septemba 29, 2019

3:00 PM AFC Leopards na Chemelil Sugar (Machakos)

3:00 PM Tusker na Sofapaka (Ruaraka)

3:00 PM Zoo na Wazito (Kericho Green)

Oktoba 5, 2019

2:00 PM Posta Rangers na Kisumu All Stars (Machakos)

3:00 PM Chemelil Sugar na Kariobangi Sharks (Chemelil Sports Complex)

3:00 PM Mathare United na Wazito (Kasarani)

3:00 PM SonySugar na AFC Leopards (Green Stadium, Awendo)

3:00 PM Western Stima na Ulinzi Stars (Moi Stadium, Kisumu)

4:15 PM KCB na Nzoia Sugar (Machakos)

Oktoba 6, 2019

2:00 PM Sofapaka na Bandari (Machakos)

3:00 PM Kakamega Homeboyz na Tusker (Bukhungu)

4:15 PM Gor Mahia na Zoo (Machakos)

Oktoba 18, 2019

3:00 PM Wazito na Kakamega Homeboyz (Machakos)

Oktoba 19, 2019

3:00 PM AFC Leopards na Western Stima (Machakos)

3:00 PM Bandari na Chemelil Sugar (Mbaraki)

3:00 PM Kisumu All Stars na Mathare United (Moi Stadium, Kisumu)

3:00 PM Nzoia Sugar na Sofapaka (Sudi Stadium, Bungoma)

3:00 PM Tusker na SoNy Sugar (Ruaraka)

3:00 PM Ulinzi Stars na KCB (Afraha Stadium, Nakuru)

Oktoba 20, 2019

3:00 PM Kariobangi Sharks na Gor Mahia (Kasarani)

3:00 PM Zoo na Posta Rangers (Kericho Green Stadium)

Oktoba 26, 2019

2:00 PM KCB na Zoo (Machakos)

3:00 PM Chemelil Sugar na Kakamega Homeboyz (Chemelil Sports Complex)

3:00 PM Nzoia Sugar na Kariobangi Sharks (Sudi Stadium, Bungoma)

3:00 PM SoNy Sugar na Kisumu All Stars (Green Stadium, Awendo)

3:00 PM Ulinzi Stars na Tusker (Afraha Stadium, Nakuru)

3:00 PM Western Stima na Bandari (Moi Stadium, Kisumu)

4:15 PM Sofapaka na AFC Leopards (Machakos)

Oktoba 27, 2019

2:00 PM Posta Rangers na Wazito (Machakos)

4:15 PM Gor Mahia na Mathare United (Machakos)

Novemba 1, 2019

3:00 PM Mathare United na Posta Rangers (Kasarani)

Novemba 2, 2019

3:00 PM Bandari na KCB (Mbaraki)

3:00 PM Chemelil Sugar na Kisumu All Stars (Chemelil Sports Complex)

3:00 PM Kariobangi Sharks na Zoo (Kasarani)

3:00 PM Tusker na Nzoia Sugar (Ruaraka)

3:00 PM Western Stima na Gor Mahia (Moi Stadium, Kisumu)

Novemba 3, 2019

2:00 PM Wazito na SoNy Sugar (Machakos)

3:00 PM Kakamega Homeboyz na Sofapaka (Bukhungu)

4:15 PM AFC Leopards na Ulinzi Stars (Machakos)

Novemba 8, 2019

3:00 PM Posta Rangers na Chemelil Sugar (Machakos)

Novemba 9, 2019

2:00 PM Sofapaka na Wazito (Machakos)

3:00 PM Kisumu All Stars na Kariobangi Sharks (Moi Stadium, Kisumu)

3:00 PM Sony Sugar na Mathare United (Green Stadium, Awendo)

3:00 PM Ulinzi Stars na Bandari (Afraha)

4:15 PM KCB na Tusker (Machakos)

Novemba 10, 2019

3:00 PM Gor Mahia na AFC Leopards (Kasarani) – ‘Mashemeji Derby’

3:00 PM Kakamega Homeboyz na Western Stima (Bukhungu)

3:00 PM Zoo na Nzoia Sugar (Kericho Green Stadium)

Novemba 20, 2019

2:00 PM KCB na Chemelil Sugar (Machakos)

3:00 PM Bandari na AFC Leopards (Mbaraki)

3:00 PM Kisumu All Stars na Wazito (Moi Stadium, Kisumu)

3:00 PM Mathare United na Sofapaka (Kasarani)

3:00 PM Nzoia Sugar na Posta Rangers (Sudi Stadium, Bungoma)

3:00 PM Tusker na Western Stima (Ruaraka)

3:00 PM Zoo na SoNy Sugar (Kericho Green Stadium)

4:15 PM Gor Mahia na Kakamega Homeboyz (Machakos)

Novemba 21, 2019

3:00 PM Kariobangi Sharks na Ulinzi Stars (Kasarani)

Novemba 24, 2019

2:00 PM Posta Rangers na Tusker (Machakos)

3:00 PM Bandari na Gor Mahia (Mbaraki)

3:00 PM Chemelil Sugar na Mathare United (Chemelil Sports Complex)

3:00 PM Kakamega Homeboyz na SoNy Sugar (Bukhungu)

3:00 PM Ulinzi Stars na Nzoia Sugar (Afraha)

3:00 PM Western Stima na KCB (Moi Stadium, Kisumu)

4:15 PM AFC Leopards na Kisumu All Stars (Machakos)

Novemba 25, 2019

2:00 PM Wazito na Kariobangi Sharks (Machakos)

4:15 PM Sofapaka na Zoo (Machakos)

Novemba 29, 2019

3:00 PM Mathare United na Kakamega Homeboyz (Kasarani)

Novemba 30, 2019

3:00 PM Kariobangi Sharks na KCB (Kasarani)

3:00 PM Nzoia Sugar na AFC Leopards (Mumias Sports Complex)

3:00 PM SoNy Sugar na Posta Rangers (Green Stadium, Awendo)

3:00 PM Wazito na Chemelil Sugar (Machakos)

3:00 PM Western Stima na Sofapaka (Moi Stadium, Kisumu)

Desemba 1, 2019

3:00 PM Gor Mahia na Ulinzi Stars (Machakos)

3:00 PM Tusker na Bandari (Ruaraka)

3:00 PM Zoo na Kisumu All Stars (Kericho Green Stadium)

Desemba 7, 2019

3:00 PM Bandari na Wazito (Mbaraki)

3:00 PM Chemelil Sugar na Western Stima (Chemelil Sports Complex)

3:00 PM Kariobangi Sharks na Tusker (Kasarani)

3:00 PM KCB na Posta Rangers (Machakos)

3:00 PM Kisumu All Stars na Gor Mahia (Moi Stadium, Kisumu)

3:00 PM Nzoia Sugar na Kakamega Homeboyz (Sudi Stadium, Bungoma)

3:00 PM Ulinzi Stars na Zoo (Afraha)

Desemba 8, 2019

2:00 PM Sofapaka na SoNy Sugar (Machakos)

4:15 PM AFC Leopards na Mathare United (Machakos)

Desemba 18, 2019

2:00 PM Sofapaka na Kisumu All Stars (Machakos)

3:00 PM Chemelil Sugar na Ulinzi Stars (Chemelil Sports Complex)

3:00 PM Kakamega Homeboyz na Bandari (Bukhungu)

3:00 PM Mathare United na Nzoia Sugar (Kasarani)

3:00 PM SoNy Sugar na Kariobangi Sharks (Green Stadium, Awendo)

3:00 PM Western Stima na Zoo (Moi Stadium, Kisumu)

4:15 PM Posta Rangers na Gor Mahia (Machakos)

Desemba 19, 2019

2:00 PM Wazito na Tusker (Machakos)

4:15 PM AFC Leopards na KCB (Machakos)

Desemba 21, 2019

3:00 PM Gor Mahia na Sofapaka (Machakos)

Desemba 22, 2019

2:00 PM KCB na Wazito (Machakos)

3:00 PM Kariobangi Sharks na Posta Rangers (Kasarani)

3:00 PM Kisumu All Stars na Bandari (Moi Stadium, Kisumu)

3:00 PM Nzoia Sugar na Western Stima (Sudi Stadium, Bungoma)

3:00 PM SoNy Sugar na Chemelil Sugar (Green Stadium, Awendo)

3:00 PM Ulinzi Stars na Kakamega Homeboyz (Afraha)

3:00 PM Zoo na Mathare United (Kericho Green Stadium)

4:15 PM Tusker na AFC Leopards (Machakos)

Januari 11, 2020

2:00 PM Posta Rangers na Ulinzi Stars (Machakos)

3:00 PM Bandari na Nzoia Sugar (Mbaraki)

3:00 PM Chemelil Sugar na Tusker (Chemelil Sports Complex)

3:00 PM Mathare United na KCB (Kasarani)

3:00 PM Western Stima na SoNy Sugar (Moi Stadium, Kisumu)

4:15 PM AFC Leopards na Zoo (Machakos)

Januari 12, 2020

2:00 PM Sofapaka na Kariobangi Sharks (Machakos)

3:00 PM Kakamega Homeboyz na Kisumu All Stars (Bukhungu)

4:15 PM Wazito na Gor Mahia (Machakos)

Januari 18, 2020

3:00 PM Kariobangi Sharks na Bandari (Kasarani)

3:00 PM Nzoia Sugar na Chemelil Sugar (Sudi Stadium, Bungoma)

3:00 PM Posta Rangers na AFC Leopards (Machakos)

3:00 PM Ulinzi Stars na Wazito (Afraha)

3:00 PM Western Stima FC vs Mathare United FC Moi Stadium, Kisumu

Januari 19, 2020

2:00 PM KCB na Sofapaka (Machakos)

3:00 PM Tusker na Kisumu All Stars (Ruaraka)

3:00 PM Zoo na Kakamega Homeboyz (Kericho Green Stadium)

4:15 PM Gor Mahia na SoNy Sugar (Machakos)

Januari 25, 2020

2:00 PM Sofapaka na Nzoia Sugar (Machakos)

3:00 PM Bandari na Tusker (Mbaraki)

3:00 PM Chemelil Sugar na KCB (Chemelil Sports Complex)

3:00 PM Mathare United na Kariobangi Sharks (Kasarani)

3:00 PM SoNy Sugar na Zoo (Green Stadium, Awendo)

3:00 PM Ulinzi Stars na Western Stima (Afraha)

4:15 PM AFC Leopards na Wazito (Machakos)

Januari 26, 2020

3:00 PM Kakamega Homeboyz na Gor Mahia (Bukhungu)

3:00 PM Kisumu All Stars na Posta Rangers (Moi Stadium, Kisumu)

Februari 8, 2020

3:00 PM Chemelil Sugar na Sofapaka (Chemelil Sports Complex)

3:00 PM Kariobangi Sharks na Kakamega Homeboyz (Kasarani)

3:00 PM KCB na Western Stima (Machakos)

3:00 PM Kisumu All Stars na AFC Leopards (Moi Stadium, Kisumu)

3:00 PM Mathare United na SoNy Sugar (Kasarani)

3:00 PM Nzoia Sugar na Zoo (Sudi Stadium, Bungoma)

Februari 9, 2020

2:00 PM Wazito na Posta Rangers (Machakos)

3:00 PM Tusker na Ulinzi Stars (Ruaraka)

4:15 PM Gor Mahia na Bandari (Machakos)

Februari 15, 2020

3:00 PM Kariobangi Sharks na Kisumu All Stars (Kasarani)

3:00 PM Sofapaka na Mathare United (Machakos)

3:00 PM SoNy Sugar na Tusker (Green Stadium, Awendo)

3:00 PM Western Stima na Chemelil Sugar (Moi Stadium, Kisumu)

2:00 PM Posta Rangers na Bandari (Machakos)

Februari 16, 2020

3:00 PM Kariobangi Homeboyz na Wazito (Bukhungu)

3:00 PM Ulinzi Stars na AFC Leopards (Afraha)

3:00 PM Zoo na KCB (Kericho Green Stadium)

4:15 PM Gor Mahia na Nzoia Sugar (Machakos)

Februari 22, 2020

2:00 PM Wazito na Western Stima (Machakos)

3:00 PM Bandari na Kakamega Homeboyz (Mbaraki)

3:00 PM Chemelil Sugar na Posta Rangers (Chemelil Sports Complex)

3:00 PM Kisumu All Stars na SoNy Sugar (Moi Stadium, Kisumu)

3:00 PM Mathare United na Zoo (Kasarani)

3:00 PM Nzoia Sugar na Ulinzi Stars (Sudi Stadium, Bungoma)

4:15 PM AFC Leopards na Tusker (Machakos)

Februari 23, 2020

2:00 PM KCB na Kariobangi Sharks (Machakos)

4:15 PM Sofapaka na Gor Mahia (Machakos)

Februari 29, 2020

3:00 PM Bandari na Mathare United (Mbaraki)

3:00 PM SoNy Sugar na Nzoia Sugar (Green Stadium, Awendo)

3:00 PM Tusker na Wazito (Ruaraka).